Connect with us

Malindi

Sam Amani, Lulu FM, Ajiunga na Redio Maisha

Published

on

Sam Amani, Lulu FM, Ajiunga na Redio Maisha pilkapilka 3

Mhariri wa habari wa kituo cha Redio cha Lulu FM Sam Amani amewaaga wafanyakazi wenzake rasmi leo Jumatatu Mei 27 ikiwa ni moja wapo ya ndoto zake ambazo zimekuwa kwenye matamanio yake.

Kupitia ukurasa wao rasmi wa mtandao wa Facebook, Lulu FM wametundika video inayomuonyesha mwendesha kipindi cha Changamka Jemimah Lauz maarufu kama Smartphone akimkabidhi Sam Amani mkate huku wakiandika maneno haya,

 Smartphone gifts Sam Amani mabofulo on his last day in office. Kila la heri katika majukumu yako mapya. #BarakaTele
#RafikiWakoWaDhati.

Kwa mjibu wa Sam ni kwamba rafiki wa karibu, Mwadanda, ambaye hakuweza kujizuia hisia zake alimwaga mtama katika mtandao wa Facebook kabla ya kuambiwa auondoe ujumbe huo na mwanahabari huyo wa Lulu FM. Ila siku chache baada ya kuondoa ujumbe huo jana aliweka mwengine akimtakia Sam kila la heri.

See also  Malindi Business & Art Exhibition by Malindians.com

‘’Nakutakia kila lakheri katika safari yako ya kujiunga na Radio Maisha kaka, Lulu Fm ndio nibasi!
CONGRATULATIONS hommie,’’ aliandika Mwadanda.

Katika post yake Mwadanda aliweka bayana kwamba Sam anajiunga na kituo cha habari cha kitaifa, Radio Maisha kituo moja wapo cha vituo vya kampuni ya Standard Media Group iliyoko jijini Nairobi.

Aidha tukiongea na Sam hakutaka kuthibitisha hilo kwa kusema kwamba cha msingi ni kwamba watu wategemee kumsikiza katika masafa ya kitaifa.

Sam alijiunga na kituo cha habari cha Lulu Fm 2016 akiwa ametoka Radio Salam alikohudumu kwa muda wa mwaka mmoja. Amewahi kukitumikia kituo cha habari cha Pamoja kwa kipindi cha miezi tisa. Anaondoka Lulu FM akiwa amefanya kazi na kampuni hiyo ya Media316 kwa takriban muda wa miaka miwili na miezi sita.

See also  Next Africa: William Ruto's Star Is Rising in Kenya - Bloomberg

Sam Amani, Lulu FM, Ajiunga na Redio Maisha pilkapilka (1)

Kulingana na mfanyikazi mwenzake Kazungu Tumaini ambaye amefanya kazi pamoja na Sam katika kituo cha Pamoja FM amesema Sam ni mchapa kazi anayejituma na hajashtushwa na kupata ajira kwake katika kampuni kubwa nchini Kenya. Amesema kwamaba Sama anandoto za kuitumikia BBC Swahili ama DW kabla ya kituo chake cha habari.

Sam ni mwanahabari wa pili kupata ajira katika moja wapo ya vituo vya kitaifa baada ya Robbie Chome kujiunga na Radio Citizen.

Sam Amani, Lulu FM, Ajiunga na Redio Maisha pilkapilka

Sam (kushoto), Jahnoh (Amka Na Rafiki Presenter) na DK(Drive Show Presenter)

Lulu FM ni kituo cha kipekee kinachopeperudisha matangazo yake kupitia mitabendi ya 97.1 Malindi na Kilifi, 91.0 Mombasa na Kwale, 106.8 Voi na Taita Taveta pamoja na 95.3 Lamu.

See also  Msanii wa Malindi Nelly Boy Kuachilia Samahani

Continue Reading
Comments
%d bloggers like this: