Connect with us

Entertainment

Msanii wa Malindi Nelly Boy Kuachilia Samahani

Published

on

samahani release pilkapilka nelly boy

Imekuwa bayana kuwa msanii Nelly Boy kutoka Malindi atakuwa akiachilia kibao kipya wiki hii kijulikanavyo kama “Samahani”. Imekuwa muda na mashabiki wake wamekuwa wakisubiri kwa hamu kujua ni lini kibao hichi kitadondolewa. Na kulingana na muujibu wa mitandao ya Kijamii, Facebook, msanii huu ameachilia poster akisema kuwa atakuwa na interview ndani ya Jahazi fm ambapo pia atakuwa akiachilia rasmi kibao hichi.

Team yetu ya Pilkapilka ilipata fursa ya kupatana naye katika studio ya Trace Records, chini na mikono ya Burning Ice. Hapa ndipo tulijua bayana kuwa kazi aliyokuwa akipika imekuwa ikitengenezwa na Trace Records. Producer Burning Ice ameathibitisha kuwa ameweka muda wake mingi katika track hii na juhudi za msanii pia zimeifanya ngoma hii kuwa kitu murua kabisa.

See also  Uko Wapi - Jaslu feat Crismatic (Video)

Pilkapilka wamepata nafasi ya kuisikiliza ngoma hii. ngoma ambayo msanii amezungumzia kuhusu kuomba msamaha wazazi wake baada ya wazazi kutoa mawaidha ambayo hayakufuatwa. Hii yote inakuja baada ya mambo kumsibu baada ya kupuuzia nasaha aliyepewa na wazazi wake.

Samahani ni wimbo ambayo iko na mafunzo kibao kwa kila mtu kuhusu kufuata nasaha za wazazi, namna ya kuishi kwenye jamii na mambo mengi. Usikose kutengea live interview ndani ya Jahazi Fm 87.7 akiwa pamoja na Host wa kipindi Jabali na Shaban aka Shampuzi siku ya Jumatano (15-05-2019)

Continue Reading
Comments
%d bloggers like this: