Connect with us

Entertainment

Msanii kutoka Watamu Lil Mizze afunguka Kuhusu Bifu yake na T buoy

Published

on

bifu ya lilmizze na t bouy.jpeg 2 pilkapilka

Kama uko na dhana ya kwamba bifu na diss track ni vitu ambavyo vimepitwa na wakati, basi mji wa watamu unagonga vichwa vya habari kwa kufufua uwepo wa diss tracks na bifu baina ya wasanii. Kupitia kwa mtandao wa kijamii Whatsapp, Msanii Lil Mizze alionyesha kughadhabishwa na matamshi ya msanii mwenzake T Buoy katika kibao cha “Snitch“. Haikutosha bali msanii huyo aliendelea na kumtaja LilMizze katika post mmoja katika mtandao wa kijamii wa Facebook.

bifu ya lilmizze na t bouy pilkapilka whatsapp status

Team ya Pilkapilka ilipata nafasi ya kuongea na Lil Mizze kwa simu ili kubaini chanzo cha bifu baina ya marafiki hao wawili. Inasemekana issue zote zilianza baada ya T Buoy kutoka kwenye game kwa muda mrefu na kupoteza touch na industry. Kwa hivyo kurudi kwake kwenye game alihitaji “promo” na kushikwa mkono na Lil Mizze ambaye kwa sasa anafanya vizuri sana kwenye game. Kipindi hicho Lil Mizze alikuwa na performance kwa Churchill Show, na T Buoy aliomba kupanda naye jukwaani. Kulingana na sheria na masharti ya performance hiyo, ilikuwa vigumu kwa Lil Mizze kukubaliana naye.

See also  Malindi Mawasco Tree planting Day

bifu ya tbuoy pilkapilka

Mambo yaliendelea kuharibika, kulingana na taarifa alizotoa Lil Mizze, T Buoy amekataa kukubali kupambana na hali ya yake haswa vile amekuwa nje ya game ya mziki kwa muda mrefu.

Jambo la kushangaza ni kuwa Deejay Nicky Phondo amekuwa akipepea moto katika bifu ya hawa wawili jambo ambalo limetuacha tukiwaza kama hii ni kiki wasanii hawa wanatafuta au kama kweli kuna issue. Pilkapilka wameweka bidii kumtafuta msanii T Buoy iliwapate ukweli wa mambo kutoka kwa upande wao.

deejay nicky fondo bifu pilkapilka

Kama unajua mengu zaidi kuhusu hii issue tujuze kwenye comments hapo chini.

Continue Reading
Comments
%d bloggers like this: