Connect with us

Malindi

Mawasco kutumia njia za kisasa za usafishaji maji

Elvis Baya

Published

on

Mawasco tree planting exercise 003

Katika Juhudi za kulinda mazingira kampuni ya Kusambaza maji mjini Malindi almaarufu Malindi Water & Sewerage Company (MAWASCO) imeanzisha mradi wa upanzi wa miti maeneo ya Sabaki kaunti ndogo ya Magarini.

Kulingana na mkurugenzi wa kampuni hiyo Gerald Mwambire, ni kwamba kupitia shirika hilo la maji wameanzisha mpango huo wa kupanda miti karibu na daraja la sabaki eneo la mto Sabaki kama njia moja wapo ya kuhifadhi mazingira huku akisema kuwa miti husaidia kuzuia mafuriko sawia na kuzuia uchafuzi wa mazingira.
Ikumbukwe kwamba mapema mwaka jana mto Sabaki ulifurika kiasi kikubwa na kusababisha hasara kwa wakaazi katika eneo hilo.

Mawasco tree planting exercise 003

Mkurugenzi Mkuu wa Mawasco, Bwana Gerald Mwambire (Aliyepiga goti)

Mwambire ameongezea kwamba hapo awali walikuwa wameanzisha mradi wa kusafisha maji taka katika eneo hilo la mto sabaki ambalo amehoji kuwa wako na sehemu ya ardhi takribani ekari 30 ambazo walikuwa wakipanda miti kila mwaka wakati mvua inapokaribia kuanza na hata mradi wa kusafisha maji taka ambao walikuwa tayari wameuanzisha hapo awali uliokuwa umegharimu kima cha pesa shilingi milioni 15 uliweza kuharibiwa na maji baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko katika sehemu ile na maeneo mengine kwenye kaunti ndogo ya Magarini.

READ  Uko Wapi - Jaslu feat Crismatic (Video)

Mawasco tree planting exercise 001

Mawasco tree planting exercise 001

Mawasco tree planting exercise 001

Aidha Mwambire ameelezea kuwa kwa sasa watatumia mbinu za kisasa ili kuhakikisha katika kuutengeneza tena mradi huo kuona kwamba hata mvua inaponyesha kubwa hauwezi kuathirika tena huku akihoji kuwa shirika lake limepanga kupanda miche takribani elfu kumi mwaka huu huku akiongeza kuwa mradi huo wa kusafisha maji taka huenda ukaanza kabla ya mwaka huu kuisha na unatazamiwa kukamilika baada ya miezi kumi na nane.

Aidha amewataka wakaazi wa eneo hilo sawia na vikundi ambavyo hujihusisha na kuhifadhi mazingira kushirikiana.
Ni kauli ambayo imeungwa mkono na Terry Michael ambaye ni mkurungenzi mkuu wa shirika la Water Services Regulatory Board (WASREB) ambaye amesema kuwa jambo hilo litasaidia pakubwa katika kuleta ustawi wa maisha ya binadamu endapo kila mwananchi atalizingatia na kulitekeleza basi huenda hali ya mazingira yakaimarika kwa kiwango kikubwa.

READ  Malindi Business & Art Exhibition by Malindians.com

Hata hivyo ameelezea kuwa miti na binadamu hutegemeana ambapo binadamu hutegemea mti kwa kupata hewa safi nayo miti hutegemea binadamu kupata hewa inayohitaji,vile vile amehoji kuwa miti husaidia kuzuia mumomonyoko wa udongo wakati mvua inaponyesha huku akiongeza kuwa ukataji wa miti kiholela au uharibifu wa mazingira unahatarisha afya ya binadamu ambapo kuna magonjwa mengi hukodolea macho binadamu kama vile ugonjwa wa ngozi(skin cancer) ambao husababishwa na kiangazi kingi.

Continue Reading
Comments
%d bloggers like this: