Connect with us

kenya

Maafisa wa Polisi wampiga risasi na kumjeruhi kijana aliyevamia Ikulu Nairobi

Avatar

Published

on

Kibet bera - mvamizi wa ikulu ya Nairobi - pilkapilka.com
Maafisa wa polisi walioshika doria na kulinda majengo ya Ikulu almaarufu  state house jijini Nairobi walilazimishwa kumpiga risasi  mwanaume aliyejaribu kufikia majengo ya Ikulu akiwa amejihami na kisu.
 
 
Kibet bera, mwanafunzi wa mitambo ya mwaka mwa tano katika chuo kikuu cha Jomo Kenyatta cha Kilimo  na Teknolojia (Jkuat), alipigwa risasi kwenye bega lake la kushoto na anapokea matibabu katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta nchini ya ulinzi mkali.
 
 
Akithibitisha taarifa hii, Kamanda mkuu wa Sub-county ya Kilimani bwana Michael Muchiri alisema jaribio hilo la kijana mwenye umri wa  miaka 25 la kujaribu kuingia Ikulu lilitokea majira ya saa kumi jioni.
 
 
Bwana Muchiri alisema maafisa waliopambana na kijana huyo Kibet wakati alivyojaribu kuingia walikuwa na changamoto ya kujaribu kumzuilia bali hakuwa na nia ya kumuua kwani ilikuwa bayana kuwa alikuwa anakaa kama alikuwa ametatizika kiakili au mwenye matatizo ya kiakili.
 
 
” Kijana huyo alipigwa risasi, kimsingi katika hali ya kumtuliza na kuondoa tishio. Shabaha ikiwa Mikono lakini kwa namna moja au nyengine alipigwa risasi kwa bega. Lakini yuko katika hali nzuri. Amelazwa kwenye hospitali ya taifa ya kenyatta na yuko nje ya hatari,” Bwana muchiri akiambia wanahabari wa Nation kwa simu.
Taarifa pia kutoka kwa Ikulu hiyo ya Nairobi pia ilithibitisha kutendeka kwa tukio hilo na kusema kuwa mwanafunzi huyo alipelekwa moja kwa moja kwenye kituo cha polisi cha Kileleshwa kabla ya kupelekwa hospitalini Kenyatta.
 
 
” Tunachukua fursa hii kuwakumbusha umma na wananchi kwamba Jumba la Ikulu ni eneo lililopangwa  chini ya sheria ya maeneo yanayolindwa nchini ya kipengele ndani ya katiba kinachojulikana kama Protected Areas Act. Kwa sababu hiyo hakuna mtu anaruhusiwa kufika majengo ya Ikulu bila kibali cha mamlaka iliyoamriwa”

READ  Decriminalizing Homosexuality
Kanze Dena-Mararo, msemaji wa Jumba la Ikulu alisema katika taarifa rasmi na wanahabari.

Hatia ya Kuingia maeneo ya Ikulu bila idhini

 
 
Bosi wa polisi alisema kuwa ni kosa la jinai kujaribu kufikia eneo lililolindwa kama Jumba la Ikulu.
 
 
” ungetozwa kwa ajili ya trespita katika eneo la usalama wa juu,” alisema.
 
 
Mwezi machi 2017, tukio kama hili lililotokea, na mtu aliyehusika huyo alipigwa risasi na kuuliwa mara moja.
 
 
Kiasi ya walinda usalama kugundua uwepo wake, alikuwa tayari ameingia ndani ya maeneo ya Ikulu hiyo na alikuwa katika eneo la maegesho ya magari.
 
 
Shambulizi hilo lilifanyika majira ya  saa kumi na moja jioni mnamo machi 25, 2017 wakati Rais Uhuru Kenyatta alikuwa akihudhuria mashindano ya golf, Muthaiga.
 
 
Maafisa wa kitengo cha huduma ya jumla(GSU) walikuwa wakipatia ulizi majengo hayo walimuua mwanaume.

READ  25 Years in Prison for Murder

Continue Reading
Comments
%d bloggers like this: