Connect with us

Entertainment

Pillar Works kuanzisha Pillar Works TV

Published

on

Pillar Works kuanzisha Pillar Works TV 4

Meneja wa Pillar Works Studio kupitia mitandao ya Kijamii ( Facebook na Whatsapp groups) ametangaza kuanzishwa kwa Stesheni ya Televisheni chini ya mwavuli wa Pillar Works hivi karibuni. Akifafanua zaidi, Tv stesheni itatambulika kama Pillar Works Tv na inakuwa ikirusha vipindi vyake katika mtandao wa Youtube na kutambulika kwa mimombo kama “Online Tv”.

“Jambo, Kwa mara ya kwanza PillarWorks Studios itakuwa inakuletea Pillarworks Tv ambayo itakuwa tunaipeperusha kupitia mtandao wa YouTube. Online Tv hii itakuwa inaangazia hasa utaarishaji wa kazi ya Msanii hususani video na audio making pamoja na behind the scenes. Vile vile itakuwa inakuletea dondo za mashabiki kutoka nyanjani na dakuzi za hapa na pale. Pillarworks Tv inakuja na kile wahitaji kufanya ni kusubscribe YouTube channel yetu ili usipitwe na lolote” – Pillar Works on Facebook

Ujumbe huu umechukuliwa vyema na wengi na kwa niaba ya kikosi kizima cha pilkapilka tunawaombea kila la kheri.

See also  Malindi Business & Art Exhibition by Malindians.com

Continue Reading
Comments
%d bloggers like this: